Mhe. Deogratius John Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na  Naibu Waziri wa Fedha Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), Rais wa Mamlaka za Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA), Mhe. Datuk Dkt. Abu Triq Jamaluddin na wadau wengine wa Mkutano wa 46 wa CATA unaofanyika jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Fedha Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb),  akieleza kuhusu matumizi ya teknolojia katika kuboresha ukusanyaji wa mapato, kurahisisha huduma kwa walipa kodi na kuongeza ufanisi wa mifumo ya usimamizi wa kodi wakati wa Mkutano wa 46 wa Wakuu wa Taasisi za Usimamizi wa Kodi na Wataalamu wa Kodi wa Mamlaka za Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA), jijini Arusha.

Wadau wa Mkutano wa 46 wa Wakuu wa Taasisi za Usimamizi wa Kodi na Wataalamu wa Kodi wa Mamlaka za Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA), wakimsikiliza Mhe. Deogratius John Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akifungua Mkutano huo, jijini Arusha.

Rais wa Mamlaka za Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA), Mhe. Datuk Dkt. Abu Triq Jamaluddin, akieleza umuhimu wa Mkutano wa 46 wa CATA, kabla ya kufunguliwa rasmi kwa Mkutano huo, jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Fedha Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb),  akiagana na  Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA Amos Makalla, baada ya kufunguliwa Mkutano wa 46 wa Wakuu wa Taasisi za Usimamizi wa Kodi na Wataalamu wa Kodi wa Mamlaka za Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA), jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Fedha Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb),  akipata maelezo kuhusu Mkutano wa 46 wa Wakuu wa Taasisi za Usimamizi wa Kodi na Wataalamu wa Kodi wa Mamlaka za Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA), kutoka kwa Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Juma Mwenda, jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Fedha Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb),  akijadili na Mwenyekiti wa Mamlaka za Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Mauritius, Sudhamo Lal, kuhusu teknolojia katika ukusanyaji wa mapato  kabla ya kufunguliwa kwa Mkutano wa 46 wa Wakuu wa Taasisi za Usimamizi wa Kodi na Wataalamu wa Kodi wa Mamlaka za Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA), jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Fedha Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb),  akijadili kuhusu maendeleo ya  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na ujumbe wa TRA ukiongozwa na  Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Juma Mwenda, katika viwanja vya  mkutano wa  Mamlaka za Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA), jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Juma Mwenda (wa pili kulia), Rais wa CATA, Mhe. Datuk Dkt. Abu Triq Jamaluddin (wa pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makalla (kushoto), na Mwenyekiti wa Bodi ya TRA, Bw. Uled Mussa, baada ya kufunguliwa kwa Mkutano wa 46 wa CATA, jijini Arusha.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)

…………….

Na. Peter Haule, WF, Arusha

Naibu Waziri wa Fedha Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), amesisitiza umuhimu wa matumizi ya teknolojia katika kuboresha ukusanyaji wa mapato, kurahisisha huduma kwa walipa kodi na kuongeza ufanisi wa mifumo ya usimamizi wa kodi.

Mhe. Munde ametoa wito huo wakati akigungua Mkutano wa 46 wa Wakuu wa Taasisi za Usimamizi wa Kodi na Wataalamu wa Kodi wa Mamlaka za Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA) unaofanyika jijini Arusha, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mhe. Deogratius John Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Munde alisema teknolojia inaendelea kubadili namna walipa kodi wanavyowasiliana na mamlaka za mapato, huku ikitoa fursa kwa Serikali kuboresha utoaji wa huduma, usimamizi wa taarifa na utii wa sheria za kodi.

“Fursa iliyopo mbele yetu ni kutumia teknolojia ili kufanya usimamizi wa kodi kuwa rahisi, wa haraka, wa uwazi na unaozingatia zaidi mahitaji ya walipa kodi,” alisema Mhe. Munde.

Alisema Tanzania inatumia mkutano huo kujifunza uzoefu wa vitendo kutoka kwa nchi nyingine wanachama wa CATA, sambamba na kushirikisha uzoefu wake katika mchakato wa kuendeleza mifumo ya kisasa ya usimamizi wa kodi na forodha.

Mhe. Munde alisema kuwa Tanzania inavutiwa zaidi na suluhisho za kiteknolojia zinazoweza kuboresha uzoefu wa walipa kodi, kupunguza gharama na  utii wa sheria, kuimarisha ubora na matumizi ya takwimu pamoja na kuongeza ufanisi wa mamlaka za mapato.

Alisisitiza kuwa thamani ya CATA ipo katika kubadilisha uzoefu wa pamoja kuwa maboresho yanayoweza kutekelezwa katika nchi wanachama.

Pamoja na maendeleo ya teknolojia, Mhe. Munde alisema misingi ya usimamizi bora wa kodi, ikiwamo haki, uadilifu na kujenga imani kwa walipa kodi, inapaswa kuendelea kupewa kipaumbele.

Aidha, Mhe. Munde aliipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Sekretarieti ya CATA na wadau wengine kwa kushirikiana katika maandalizi ya mkutano huo.

Tanzania inakuwa mwenyeji wa mkutano huo kwa mara ya kwanza, jambo ambalo Munde alisema ni heshima kubwa kwa nchi na ishara ya imani iliyowekwa na uongozi wa CATA pamoja na mamlaka za kodi wanachama.

 

Mkutano huo unafanyika Tanzania ukiwa na lengo la kuimarisha ushirikiano wa kitaalamu miongoni mwa mamlaka za kodi na kujadili mikakati ya kutumia teknolojia kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato.

Mkutano huo wenye kaulimbiu “Leveraging Technology for Efficient Revenue Collection”, umehudhuliwa na Rais wa CATA, Mhe. Datuk Dkt. Abu Triq Jamaluddin, pamoja na Mwenyekiti wa CATA na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Mauritius, Sudhamo Lal, Mkurugenzi Mtendaji wa CATA, Dkt. Esther Koisin, na Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Juma Mwenda.

Mkutano huo pia umewakutanisha Makamishna Wakuu na Wakuu wa Mamlaka za Kodi kutoka nchi mbalimbali wanachama wa Jumuiya ya Madola, kwa lengo la kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano na kutumia teknolojia kuboresha ukusanyaji wa mapato.