Dar es Salaam iliwaka wakati vijana wenye vipaji mbalimbali walipokutana katika usaili wa Serengeti Lite Nyota Bigi Msimu wa Pili, wakipewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao na kung’arisha vipaji walivyonavyo.
Usaili huo umewakutanisha vijana wenye vipaji vya kuimba, kucheza, kuigiza, kuchekesha, uanamitindo pamoja na ubunifu mwingine mbalimbali, na kuwaweka katika jukwaa moja ili waonyeshe uwezo wao mbele ya watazamaji na wataalamu wa tasnia.
Kupitia ushirikiano na KUNTA Africa, Serengeti Lite inaendelea kutoa nafasi kwa vijana kuamini vipaji vyao, kuvitumia na kufikiria zaidi kupitia kaulimbiu yake ya “Lite Your Imagination.”
Baada ya Dar es Salaam, safari ya kutafuta Nyota Bigi inaendelea katika miji ya Arusha, Dodoma na Mwanza, ambako vijana wengine watapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na kuwania nafasi ya kuwa Nyota Bigi wa msimu huu.
Nani ataibuka kuwa Nyota Bigi? Safari bado inaendelea.

