Mradi wa Upanuzi na Usambazaji wa Maji katika vijiji 11 vinavvyozunguka Mgodi wa Barrick North Mara, unaogharimu kiasi cha shilingi Bilioni 2,665,052,934,46 Umekabidhiwa kwa serikali na mgodi wa Barrick North Mara ambao utahudumia wananchi 94,696 na kwa sasa unahudumia wananchi 47,696.

Akizungumza meneja wa Ruwasa wilaya ya Tarime mhandisi Leo Resicius amesema awamu hii ya pili ya Mradi umeongeza uzalishaji kutoka lita Milioni 2,314,000 kwa siku hadi kufikia lita milioni 10,213,00 ukiwa na lengo la kumpunguzia changamoto ya ukosefu wa maji kwa wanawake 

Mradi huo ni awamu ya pili ya utekelezaji ambapo kukamilika kwa mradi huo ni ushuhuda mwingine wa jinsi Mgodi wa North Mara unavyotekelezaj azma yake ya kuwa mshirika wa maendeleo kwa jamii inayozunguka mgodi huo.

Kwa uapnde wake meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara Apolinary Lyambiko amesema kama Barrick wanajivunia kuwa sehemu ya kutekeleza Azma ya serikali ya wananchi kupata huduma ya maji safi na salama.

Kupitia program za uwajibikaji kwa jamii mgodi CSR umekuwa ukitenga bilioni 4 kwa mwaka kwajili ya uwekezaji kwenye miradi ya Elimu,Afya ,Barabara mazingira na uwezeshaji kiuchumi ambapo kuanzia mwaka 2019-2025 bilioni 31 zimewekwazwa katika miradi mbalimbali ambapo miradi 250 imewekezwa.

Aidha Akizindua mradi huo mkuu wa wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele amewataka wananchi kulinda vyanzo vya maji katika eneo hilo nakulinda uwekezaj mkubwa wa mgdoi ambao umekuwa ukisaidia upatikanaji wa huduma.