Na Sixmund Begashe, Moshi 

TIMU ya Maliasili Wanawake (KE) Mchezo wa Kamba imewainua mashabiki wake wa Mkoa wa Kilimanjaro na mikoa ya jirani kwa shangwe kubwa baada ya kuiburuza timu ya Vijana 2-0 katika mtifuano mkali wa Michezo ya SHIMIWI 2026, kwenye viwanja vya Chuo cha Polisi (CCP) Moshi.

Katika mchezo huo wa kuingia 8 bora, mvuto wa kwanza wa timu hiyo iliyosheheni wachezaji wenye nguvu mithili ya Faru wa Hifadhi ya Taifa Mkomazi, walitumia sekunde 4 kuwabagaza wapinzani wao. 

Akizungumzia mchezo huo, Kocha wa timu hiyo Bw. Gabriel Michael, amesema siri ya ushindi ni maandalizi mazuri waliyofanya huku Nahodha wa timu hiyo Bi. Tatu Chacha akiahidi ushindi zaidi katika michezo inayofuata.