Vijana wameaswa kuhakikisha wanakuwa na uzalendo na kutunza amani katika nchi yao ikiwa pamoja na kuachana na tabia ya kukaa vijiweni na badala yake wajitokeze kwa wingi katika kushiriki kikamilifu katika michezo mbali mbali lengo ikiwa ni kujenga afya na kuondoikana na magonjwa yasiyoambukizwa.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa vijana (UVCCM) Wilaya ya Kibaha mjini Ramdhani Kazembe kwa alipokiuwa mgeni rasmi katika Bonanza la Tangini kwa niaba ya mjumbe wa kamati ya siasa ya Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa wa Pwani Alhaj Mussa Mansour.
Pia Kazembe amesema kwamba Alhaj Mansour ameahidi kushirikiana bega kwa bega na viongozi wa Jogging zote za Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha na kwamba atajipanga kukutana nao kwa ajili ya kuweka mikakati madhubuti ambayo itaweza kusaidia kwa kiasi kukibwa katika kusapoti mchezo huo pamoja na kuitimia fursa hiyo katika suala zima la kupata a mikopo ya asilimi 10 ambayo inatolewa na Halmashaur kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi.
“Napenda kuwapongeza kwa dhati wanachama wa Tangini Jogging pamoja na vilabu vyote ambavyo vimeweza kushiriki kikamilifu katika bonanza hili na kwamba mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM Moa wa Pwani ameniagiza kuja kwa ajili ya kumwakilisha na kwamba amesema yupo pamoja na nyinyi na kwamaba ataendelea kushirikiana na vijana katika kuendeleza klabu za Jogging,”amebainisha Kazembe.
Kwa upande wake mratibu wa Bonanza hilo la Tangini seoson One Ally Gombati amesema kwamba lengo kubwa la kufanyika kwa bonanza hilo ni kwa ajili ya kushirikisha vilabu vingine vya Jogging kwa lengo le kufanya mazoezi ili kujenga na kuimraisha afya ikiwa sambamba na kuunga juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya michezo,
Mratibu Gombati amebainisha kwamba wameona ni muhimu katika kuwaunganisha vijana kwa pamoja ikiwa ni katika kuweka misingi imara ikiwa pamoja na kuwakumbusha umuhimu wa kulinda amani ya nchi yao pamoja na umuhimu wa kufanya mazoezi ili kujenga afya zao,
“Tumeamua kuandaa bonanza hili ambalo tumeliita jina la Tangini bonanza na tumeweza kuvishirikisha vilabu la Jogging zaidi ya 30 kutoka maeneo mnnbali mbali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha pamoja na maeneo mengine jirani ya Jiji la Dar es Salaam ikiwemo E-FM Jogging,Clouds Jogging, Tangini Jogging pamoja na Jogging nyingine kutoka sehemu mbali mbali,”amebainisha Mratibu Gombati.
Nao baadhi ya wanachama wa Tangingini Jogging club wamesema kwamba tamasha hilo limeweza kuwapa fursa ya kufahamiana na watu kutoka maeneo mbali mbali na kwamba mazoezi hayo yataweza kuwasaidia kwa kiais kikubwa katika kuimraisha afya zao na kuondokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza pamoja na kundoa kitambi.
“Kwa kweli sisi tuanpenda kutoa shukrani zetu za kipekee kwa uongozi wa Tangini kwa kuona umuhimu wa kuweza kuandaaa bonanza hili ambalo limeweza kutukuzanisha na wenzetu kutona maeneo mbali mbali ya kutoka Wilaya ya Kibaha pamoja na maeneo mengine ya Jijiji la Dar es salaam na hakika tumeweza kukimbia pamoja na kubadilishana mambo mbali mbali ya michezo ikiwa pamoja na masuala ya kimaendeleo,”amebainisha baadhi ya wanamichezo hao.
Bonanza la Tangini Season One limefanyika na kuwajumisha vilabu mnbali mbali kutoka katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha pamoja na vilabu vingine vya Jogging kutoka maeneo ya Jiji la Dar es Salaa kwa lengo la kuweza kuweza kutengeneza urafiki, kudumisha hali ya umoja na mshikamano pamoja na kuimarisha afya na mwili pamoja na kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambukizwa.

