………
Na Mwandishi Maalumu RS Arusha
TIMU ya RAS Arusha imeanza vyema mashindano ya Shimiwi yanayofanyika mkoani Kilimanjaro, baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa na Sadick Nangi, na kuiwezesha RAS Arusha kuondoka na pointi tatu muhimu katika mashindano hayo yanayoshirikisha timu kutoka taasisi mbalimbali za Serikali.
Mashindano ya Shimiwi yanafanyika mkoani Kilimanjaro, yakilenga kuwakutanisha watumishi wa Serikali katika michezo mbalimbali.