Na Sixmund Begashe, Moshi
MALIASILI Sports Club kupitia timu zake za Kamba Wanaume (ME) na ya Wanawake (KE) imezidi kuweka historia kwa kuzidondoshea kipigo kizito timu pinzania inazo kutana nazo kwenye michezo ya SHIMIWI 2026, Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Katika michezo iliyowavutia mashabiki wengi, Maliasili Kamba KE iliiburuza timu ya Wizara ya Madini Kamba KE na kuibuka na ushindi wa 2-0 huku timu ya Maliasili Kamba ME ikitumia sekunde 5 kuibagaza timu ya RAS Kagera Kamba ME kwa ushindi wa 2-0.
Akizungumzia ubabe wa timu za Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Chuwa Beno mkazi wa Kibosho Kirima, amesema anaona ushindi mkubwa mbeleni kwa Club hiyo kongwe, maana ni kama haina mpinzani.

