*Aagiza kukamatwa kwa familia ya Mushi kutokana na kushindwa kufika eneo la tukio.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameagiza familia ya Devid Mushi kukamatwa na kufikishwa kituo cha polisi cha Oysterbay hadi siku ya jumatatu septemba 21,2026 baada ya kudharau wito wake alipotembelea eneo la mtaa wa Madale wilaya ya Kinondoni ulipokuwa mgogoro wa ardhi baina ya familia hiyo na familia ya Abdallah Msham Kitwanga
RC Chalamila ametoa agizo hilo mara baada ya kufika kwenye eneo hilo la wananchi zaidi ya kaya 15 walioathiriwa na mgogoro wa ardhi unaohusisha familia za marehemu Abdallah Msham Kitwanga na Marehemu na Devid Mushi kwenye mtaa wa madale wilaya ya Kinondoni ambao waliondoshwa kwenye nyumba zao na kutolewa vyombo vyao nje tokea septemba 3 ,2026 kufuatia familia ya Devid Mushi kupata ushindi wa kesi ya mgogoro huo mahakamani lakini familia hiyo ya Devid Mushi haikutii kuwepo eneo hilo.
Akizungimza mara baada ya kufika kwenye eneo hilo la mgogoro Chalamila amesema alitoa taarifa ya kufika kwenye eneo hilo ili akutane na familia zote mbili za mgogoro huo pamoja na wahanga lakini familia ya Devid Mushi imedhatau wito huo huku akisisitiza kuwa hakuwa na mpango wa kuvunja hukumu iliyotolewa na mahakama bali alitamani kuwakutanisha ili kama itaawezekana kuwe na maridhiano ya wananchi kuweza kununua maeneo hayo
Aidha RC Chalamila amesema amehuzunishwa na kitendo cha familia hiyo kutotii maelekezo na ameendelea kuweka msisitizo wa marufuku kwa mabaunsa kutumika kwenye migogoro ya ardhi kwa kuwa hawana mafunzo husika badala yake jeshi la polisi ndio litumike
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Saad Mtambule ameeleza kiini cha mgogoro huo kuwa hapo awali mwaka 2015 Abdallah Msham Kitwanga alipeleka shauri hilo mahakamani dhidi ya Devid Mushi na kupata ushindi na baadaye kuwauzia wananchi maeneo hayo.
Vilevile Mtambule ameongeza kuwa baada ya wananchi kununua na kujenga nyumba zao baadae familia ya Devid Mushi ilipeleka shauri hilo tena mahakamani na kupata ushindi mwaka 2022 na ndipo wananchi hao zaidi ya kaya 15 kuanza kusimbuliwa wakitakiwa kuondoka na kumekuwa na mazungumzo mara kadhaa ili kufikia suluhu ya sakata hilo.
Nao baadhi ya wananchi waliopata fursa ya kuongea mbele ya Mkuu wa Mkoa wameiomba Serikali kuwasaidia kufikia maridhiano ili walipie ardhi kwa bei itakayoridhiwa na pande zote

