Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Nyakia Ally chirukile wakati akizungumza na wahitimu wa mafunzo kikosi cha 846 JKT Luwa iliyopo Manispaa ya Sumbawanga.
Na Neema Mtuka , Sumbawanga Rukwa:
Vijana wa Kundi lazima oparesheninishati safi na kundi la kujitolea oparesheni Linda amani wametakiwa kutumia Elimu walio ipata katika Mafunzo yao kujikwamua kiuchumi na kutoa dhana ya kupata ajira katika Majeshi nchini.
Wito huo umetolewa Septemba 14 ,2026 na Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga Nyakia Ally chirukile ambaye ndiye mgeni rasmi wakati wa kuhitimisha mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa vijana hao katika kambi ya jeshi 846 JKT Luwa iliyopo Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Kwa upande wake Kamanda wa kikosi cha Jeshi 846 Luwa Brigedia Javan Josephat Gwai amesema vijana hao wamejifunza mbinu mbalimbali za kujiinua kiuchumi ikiwemo kilimo,ili kuwajengea uwezo wa Kujiajiri.
Hata hivyo mwakilishi wa mkuu wa Majeshi Nchini jeneral Jacob John Mkunda Brigedia Soletina Bernard Mshusi mkurugenzi wa ustawi wa jamii jeshini amewataka kuwa vijana bora katika jamii kwa kujiepusha na vitendo vitakavyo dhoofisha afya ya akili na mwili.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya amewataka vijana kutojihusisha au kujiunga na vikundi vya uhalifu na madawa ya kulevya.
Akisisitiza vijana hao kutumia vyema mitandao ya kijamii badala yake wakawe mabalozi wema katika Jamii.
Baadhi ya vijana waliohitimu mafunzo hayo akiwemo Raymond machesha kutoka mkoani Geita amesema atatumia mafunzo hayo kuwa balozi mzuri wa kuelimisha jamii kuhusu uraia ,uzalendo na nishati safi.
Baadhi ya vijana waliohitimu kundi la kujitolea oparesheni Linda amani na kikosi cha kujitolea oparesheni nishati safi kikosi cha 846 JKT Luwa iliyopo Manispaa ya Sumbawanga
