Mkuu wa wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali Akiongea katika kikao hicho kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere .

 Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania ( TCRA)Mhandisi Peter Mwasalyanda wakati akizungumza katika kikao kilichowakutanisha wadau kujadili uhalifu mitandaoni.

Baadhi ya wadau walioshiriki katika kikao hicho cha kujadili uhalifu mitandaoni

Na Neema Mtuka, Sumbawanga

RUKWA: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo, Septemba 10, 2026, imewakutanisha wadau mbalimbali mkoani Rukwa, wakiwemo watoa huduma za mawasiliano ya simu, sekta ya usafiri, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na makundi mbalimbali ya kijamii, kwa lengo la kujadili namna ya kukabiliana na kutokomeza uhalifu wa mtandaoni unaoendelea kushika kasi mkoani humo.
Akifungua mkutano huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali, amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa na kuripoti vitendo vya uhalifu wa mtandaoni, ikiwemo kuwabaini na kuwafichua wahalifu waliopo katika maeneo yao.
“Tushirikiane kwa pamoja katika kutokomeza uhalifu wa mtandaoni Rukwa. Bila matukio haya, inawezekana; nguvu ya pamoja inahitajika,” amesema Lijualikali.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi Peter Mwasalyanda, amesema bado kuna mwendelezo wa vitendo vya uhalifu vinavyofanyika kupitia huduma za simu na intaneti, huku Mkoa wa Rukwa ukiendelea