Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Florence Samizi, ametoa elimu kwa mama wa mapacha watatu, Maridhia Miraji, kuhusu namna bora ya kuwahudumia watoto hao ili waweze kukua vizuri, ikiwemo kuzingatia usafi, lishe na kinga dhidi ya maambukizi.

Dkt. Samizi amemuelekeza mama huyo namna ya kuwahudumia watoto njiti, hususan kuhakikisha wanapata joto la kutosha, lishe sahihi na uangalizi wa karibu, pamoja na kufuatilia afya zao kwa mujibu wa ushauri wa wataalamu wa afya.

Amesema malezi na uangalizi mzuri kwa watoto njiti ni muhimu katika kuhakikisha wanakua salama na kufikia hatua nzuri za ukuaji na maendeleo.