• Wateja wa Shangwe Kutesa na EPL
• Wale wa Compact kupata mserereko wa UEFA
USIWAZE – ndio ofa mpya iliyotangazwa na MultiChoice Tanzania, inayowawezesha wateja wanaostahili wa DStv kupata kifurushi cha juu zaidi kwa gharama ya kifurushi chao cha sasa kwa muda maalum.
Ofa hii itakayodumu kwa zaidi ya mwezi mmoja itaanza Septemba 7 hadi Oktoba 19, 2026 ambapo katika kipindi hicho mteja akilipia kifurushi chake, ataweza kushuhudia maudhui ya kifurushi cha juu yake.
Wateja wapya, wanaotumia huduma kwa sasa, pamoja na wale ambao vifurushi vyao vilishakatika watanufaika na ofa hii punde tu watakapolipia vifurushi vyao – na hivyo kupata moja kwa moja maudhui ya kifurushi kinachofuata juu ya kile wanacholipia, bila gharama yoyote ya ziada.
Akizungumzia ofa hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania, Godfrey Bwana, alisema, “Ofa hii ni kuwathibitishia wateja wetu kuwa tunawathamini na hivyo kuwapa fursa ya kufurahia zaidi burudani za kiwango cha aina yake, ikiwemo michezo, filamu, tamthilia, makala maalum, vipindi vya watoto, habari pamoja na maudhui ya ndani, huku tukiendelea kuwapa huduma ya hali ya juu.
Kwa wale wapenzi wa kandanda ofa ya Usiwaze itawatoa kimasomaso kwani mteja wa kifurushi cha Shangwe cha Tsh 40,000 akilipia kifurushi chake sasa ataweza kushuhudia ligi kuu ya Uingereza, wakati yule wa kifurushi cha Compact cha 68,000 akilipia kifurushi chake ataweza kushuhudia michuano ya UEFA katika kipindi chote cha ofa.
Wale wa Compact plus nao wakilipia kifurushi chao wataweza kushuhudia maudhui ya kifurushi cha juu kabisa cha DStv Premium katika kipindi hicho cha ofa.
Kwa wapenzi wa tamthilia na maudhui ya kibongo wa kifurushi cha Poa cha Tsh 10,500 nao wakilipia kifurushi chao, wataweza kupata uhondo wa chaneli ya Maidha Magic Bongo wakati wote wa kipindi cha ofa
Baada ya muda wa ofa kukamilika, wateja wote watarejeshwa moja kwa moja kwenye kifurushi walichokuwa wamejisajili na kukilipia.
Promo hii inapatikana kwa wateja wa DStv wa matumizi ya nyumbani, ikiwemo wateja wapya na wale wanaorejesha huduma baada ya kukatwa. Hata hivyo, wateja wa DStv Premium, DStv Stream, DStv Business, akaunti maalum, pamoja na wateja wanaotumia baadhi ya vifurushi vya nyongeza vinavyojitegemea
