Jumla ya wasicha 25 kutoka Zanzibar na mikoa ya Kilimanjaro na Dar es salam wanufaika na program ya “The Hope Atelier – Fashion for Empowerment”, hii ni programu ya uwezeshaji wasichana vijana wenye umri wa miaka kati ya 16 hadi 30, hususan wanaotoka katika mazingira yenye changamoto za kiuchumi na wenye shauku ya kujifunza ubunifu wa mitindo na ushonaji wa nguo za aina mbalimbali, mafunzo hayo yalianza tarehe 20 Julai 2026 chuo cha VETA Dar es salaam na yatahitimishwa tarehe 4 Septemba 2026.
Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka na Elimu ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) CPA. Athony Kasore aliwatembelea wasichana hao tarehe 28 Agasti, 2026 chuoni hapo na kujionea kile walichojifunza katika sekta ya ubunifu na mitindo ya mavazi wakiwa chuoni hapo kupitia programu maalum ya “The Hope Atelier- Fashion for Empowerment iliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Fashion for Empowerment (F4E) ya nchini india na Sisters in Iman (SII) ya Tanzania.
“napenda kuwapongeza sana nimepita hapa kwenye karakana na kujionea bunifu mbambali ikiwemo nguo zilizoshonwa kwa vitambaa vya kanga,mikoba iliyo fumwa kwa nyuzi, kofia zilizonakshiwa kwa rangi na maua yakuvutia na bidhaa nyingine nyingi zilizotokana na mawazo yenu ya kibunifu” Amesema Kasore.
Kasore ameedelea kuwahamasisha wasichana hao kuendelea kutumia ujuzi wao ili waweze kujiajiri, kuajiri wengine na hatimaye kujipatia kipato hivyo kujiimarisha kiuchumi.
Kwa upande wake Dkt Salma Iddy ambaye ni mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Sisters in Iman amesema kupitia programu hiyo washiriki wamepata mafunzo ya ushonaji wa mavazi ya aina mbalimbali, kudarizi, kufuma mikoba kwa kutumia nyuzi na bidhaa nyingine, pamoja na ujasiriamali, elimu ya fedha na stadi za maisha.
“Lengo letu ni kuwajengea wasichana ujuzi wa vitendo, kujiamini na uwezo wa kubadilisha vipaji vyao kuwa biashara au ajira endelevu na kujikwamua kiuchumi lakini tunatarajia kuwaona wakihitimu kama wabunifu chipukizi, wakianzisha biashara zao, kutengeneza kipato na kujitegemea kiuchumi.
Dkt Salma ameongeza na kusema kuwa “hata hivyo tunalenga kuendeleza The Hope Atelier kwa kuanzisha kituo (hub) ambayo itawapa wahitimu hawa nafasi ya kuendelea kuzalisha bidhaa, kupata uzoefu na kufikia masoko mbalimbali”
Aidha Dkt Salma amehitimisha kwa kumshukuru Mkurugenzi Mkuu kwa kutenga muda wake na kwenda kuwatembelea wasichana hao nakuona kazi zao mbalimbali za kibunifu, ameongeza na kusemakuwa ujio huo umewapa nguvu zaidi ya kuendeleza maono ya “The Hope Atelier”.

