Na Victor Masangu, Kibaha
Baadhi ya wanawake wa (UWT) Kata ya Pangani iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha  wamempongeza kwa dhati Mwenyekiti  wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini Elina Mgonja  kwa kuamua kutekeleza  aahadi yake kwa vitendo kwa  kufanya ziara maalumu kwa lengo la  kwenda kutoa  mafunzo maalumu  kwa ujasiriamali   ya kuweza  kutengeneza bidhaa za aina mbali mbali ili  kuweweza  kujikwamua kiuchumi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya Mwenyekiti huyo wa UWT Wilaya ya Kibaha Mwenyekiti wa UWT Kata ya Pangani  Johari Komba amebainisha kwamba wamefarijika sana kupata fursa hiyo ya  kupata ujuzi mbali mbali na kufundishwa  jinsi ya kutengeneza bidhaa  tofauti ikiwemo jinsi ya kutengeneza sabuni pamoja na ubunifu wa  batiki.

“Kwa kweli sisi kama wanawake wa UWT  kata ya Pangani tunapenda  kumshukuru kwa dhati Mwenyekiti wetu wa Wilaya mama yeetu Elina Mgonja kwa kuweza kuamua kutekeleza ahadi yake kwa vitendo ya kuja kututembelea katika Kata yatu na  haya mafunzo yataweza kutusaidia kwa kiasi kikubwa wanawake kuweza kujikwamuaa kiuchumi,”amebainisha Mwenyekiti huyo.

Mwenyekiti huyo amesema kwamba  fursa za kupatiwa mafunzo hayo itakuwa ni  moja ya mkombozi mkubwa ya kuweza kujifunza mbinu na ujuzi mbali mbali wa namna ya kuweza kujifunza namna ya kutengeneza bidhaa hizo ambazo zitaweza kuwasaidia kuondokana na wimbi la umasikini na kuleta chachu ya maendeleo.

Naye mmoja wa wananawake  wajasiriamali kutoka kata ya Pangani Rehema Seleman ambaye ameweza kunufaika kwa  kiasi kikubwa na mafunzo  ambayo alipatiwa na Mwenyekiti huyo wa UWT Wilaya ya Kibaha katika kipindi  cha nyuma hakusita kueleza mafanikio ambayo ameweza kuyapata ikiwemo  suala la kuanzisha miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo kuwepo na kujenga makazi ya kuishi kupitia shughuli za ujasiriamali.

“Mimi niliweza kupata fursa ya mafunzo mbali mbali kutoka kwa Mwenyekiti wetu wa Jumuiya ya wanawake wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini  na leo hii nashukuru nimepata mafanikio makubwa sana ikiwemo nimeweza kujenga nyumba yangu na mambo mengine mbali mbali nimefanya ya kimaendeleo kwa hiyo mwalimu wangu Elina Mgonja ameweza kunitoa mbali sana katika kunipa ujuzi na maharifa,”amebainisha Rehema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini Elina Mgonja amesema kwamba ameamua  kufanya ziara hiyo ya kuweza kutoa mafunzo hayo ya ujasiriamali kwa wanawake wote wa UWT kutoka kata zote 14 zilizopo katika Halmashauri ya manispaa ya Kibaha.

Mwenyekiti huyo amesema kwamba kufanyika kwa ziara hiyo ni moja ya utekelezaji wa ahadi yake ambayo aliitoa kwa wanawake akiwa katika ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kuwashukuru kwa kukipigia kura za kishindo kwa viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) katika nafasi za udiwani,Ubunge pamoja na nafasi ya Rais katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2025.