Mabigwa Watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga SC, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo, Agosti 16, 2026, kwenye Uwanja wa Majaliwa, mkoani Mtwara.
Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Chadrack Boka, Max Nzengeli pamoja na Peter Shalulile, huku bao la kufutia machozi la Namungo likifungwa na Helbert Lukindo.
