Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo, Agosti 16, 2026, mkoani Kagera.
Kufuatia ushindi huo, Simba SC imefanikiwa kukusanya pointi tatu muhimu katika mchezo wake wa kwanza wa mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
