Na Hellen Mtereko,Mwanza

Katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri ya mfumo wa maji ulio safi, salama na wakudumu Kampuni ya VEROTAS PLUMBING imeendelea kutoa huduma hiyo muhimu kwa kuuza bidhaa ambazo zina ubora.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa VEROTAS PLUMBING, Veronica Mwita, amesema kampuni hiyo imejikita katika kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa na huduma zinazowawezesha kuwa na mifumo bora ya maji katika mazingira yao.

Amesema matumizi ya bidhaa bora katika mfumo wa maji ni muhimu katika kuhakikisha maji yanapitishwa kwenye mazingira salama, huku yakipunguza changamoto zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya vifaa visivyo na ubora.

“Tunatoa suluhisho kwenye mifumo ya maji kwa kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa zenye ubora ambazo zitawasaidia kuwa na mfumo mzuri, salama na wa kudumu,tunazingatia mahitaji ya wananchi kuanzia kwenye maliwato hadi kwenye mfumo mzima wa maji wa nyumba,” amesema Mwita.

Aidha, amesema VEROTAS PLUMBING inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kuchagua bidhaa sahihi wakati wa kujenga au kuboresha mifumo ya maji, ili kuepuka gharama zinazoweza kujitokeza kutokana na uharibifu wa mifumo.

Amesema wananchi wanapaswa kuzingatia ubora wa bidhaa wanazonunua na kuhakikisha zinafaa kwa matumizi yanayokusudiwa, kwani mfumo bora wa maji una mchango mkubwa katika usafi, afya na ustawi wa familia.

VEROTAS PLUMBING imeendelea kuwahimiza wananchi wanaojenga nyumba mpya au kufanya maboresho katika nyumba zao kutumia wataalamu na bidhaa bora ili kuhakikisha mifumo ya maji inakuwa salama, imara na yenye kudumu kwa muda mrefu.