Na Victor Masangu, Kibaha
Jumuiya  ya  umoja wa wanawake  (UWT) Wilaya ya Kibaha  mjini kwa kushirikiana na wadau  wengine  wa  maendeleo  wakiwemo  Azania bank  wameamua kuungana  kwa  pamoja   na kuitoa darasa la mafunzo kwa wajasiriamali  kutoka kata  zote 14  kwa lengo  la kuweza kuwapa ujuzi wa kutengeneza bidhaa mbali mbali ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza  katika ziara  maalumu ya kikazi  yenye lengo la kuweza kutoa mafunzo hayo Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini Elina Mgonja amebainisha kwamba ameamua kutoa darasa hilo ikiwa ni ahadi yake ambayo aliitoa wakati wa zira  ya kushukuru wanawake  kwa kuweza kuipigia CCM  kura za kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Mwenyekiti Mgonja amesema kwamba ametembelea  wanawake hao na kutoa fursa za mafunzo ya ujarisiamali kwa kuwafundisha jinsi ya kutengeneza bidhaa za aina tofauti zikiwemo  utengenezaji wa sabubi  kwa ajili ya  kufulia nguo , sabuni ya kuogea, na namna ya kutengeneza batiki pamoja na utengenezaji wa bidhaa nyingine.
“Nikiwa kama Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini nimeamua kutimiza ahadi yangu ya kuwapa mafunzo ya ujariamali bure wanawake kutoka kata  zote 14   zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha na mafunzo haya pia nimeshirikiana na wenzetu wa Azania bank ambao na wao wameweza kutoa elimu ya jinsi ya kutunza fedha na kujikwamua kiuchumi,”amebainisha Mwenyekiti Mgonja.
Kwa upande wake Afisa  Mahusiano wa Azania Bank Happiness Lema  amebainisha kwamba lengo lao kubwa la kushirikiana bega kwa bega  na Jumuiya ya ya wanawake wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini kwa lengo la kuwasaidia  kuwapa  elimu  ya kujikwamua kichumi ikiwemo pamoja na suala zima la utunzaji wa fedha.
“Sisi kama Azania bank tumeoana kuna umuhimu mkubwa wa kuweza kushirikiana na Jumujiya ya wanawake wa UWT Wila ya Kibaha mjini na tumeamua kutembea nao katika ziara yakeo yenye lengo la kutoa darasa maaalumu kwa ajili ya kuwafundisha jinsi ya kutengeneza bidhaa na sisi kama benki  tumewafundisha namna bora ya kujikomboa kiuchumi pamoja na jinsi ya kutumia fursa za mikopo yenye liba nafuu,”amenainisha Happiness.
Ziara ya Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini ya kutoa mafunzo kwa wanawake wajasiriamali  kwa sasa inaendelea kufanyika ambapo hadi sasa imeshapita katika kata tisa ambazo ni Msangani, Mkuza, Maili moja, Tumbi, Viziwaziwa, Kibaha, Kongowe,  Misugususgu pamoja na Kata ya Visiga.