Afisa Kilimo wa Abatop Prime Limited, inayojulikana kama Asteria Agrovet, Zuhura Yusuf akizungumza kwenye maonesho hayo jijini Arusha

Happy Lazaro,Arusha.

Arusha .Abatop Prime Limited inayojulikana kama Asteria Agrovet ambao ni wauzaji wa pembejeo za kilimo wameshiriki katika maonyesho ya Nanenane na kuwafikia idadi kubwa ya wakulima kwa kuwaelimisha kuhusu bidhaa mbalimbali za kilimo zenye ubora wa hali ya juu na matokeo makubwa .

Akizungumza katika maonesho hayo Afisa Kilimo wa Abatop Prime Limited, inayojulikana kama Asteria Agrovet, Zuhura Yusuf, amesema ushiriki wao ni sehemu ya juhudi za kampuni kuhakikisha wakulima wanapata fursa ya kuzifahamu bidhaa mbalimbali wanazohitaji katika shughuli zao za kilimo.

Amesema kuwa ,Asteria Agrovet imekuja na bidhaa tofauti zinazolenga kukidhi mahitaji ya wakulima katika hatua mbalimbali za uzalishaji, huku akiwataka wananchi wanaotembelea maonesho hayo kufika katika banda lao ili kupata elimu na maelekezo kuhusu matumizi sahihi ya bidhaa hizo.

Zuhura amesema kuwa,maonesho ya Nanenane ni fursa muhimu kwa wakulima kukutana na wataalamu wa kilimo, kujifunza teknolojia na bidhaa mpya, pamoja na kupata ushauri unaoweza kuwasaidia kuongeza tija katika uzalishaji.

Ameongeza kuwa Asteria Agrovet inaendelea kutoa elimu kwa wakulima ili kuhakikisha wanatumia bidhaa za kilimo kwa usahihi na kwa kuzingatia mahitaji ya mazao yao, jambo litakalosaidia kuongeza uzalishaji na kuboresha kipato.

“Wakulima wanaofika katika banda la Asteria Agrovet katika Maonesho ya Nanenane wanapata nafasi ya kuuliza maswali, kupata ushauri kutoka kwa wataalamu na kufahamu bidhaa zinazoweza kuwasaidia katika shughuli zao za kilimo.”amesema .

Zuhura amewakaribisha wakulima na wananchi kwa ujumla kutembelea banda la Asteria Agrovet katika maonesho ya Nanenane ili kupata elimu zaidi kuhusu bidhaa zao na namna zinavyoweza kutumika kuboresha uzalishaji wa kilimo.

Ameongeza kuwa ,kupitia maonesho hayo wamepata fursa ya kuweza kuwaonyesha wakulima bidhaa mbalimbali za kilimo zenye ubora wa hali ya juu, huku ikiwahakikishia upatikanaji wa pembejeo muhimu kwa ajili ya kuongeza tija katika uzalishaji.

Zuhura amesema Asteria Agrovet ina mbegu za aina mbalimbali zikiwemo Hybrid na OPV, kwa mazao tofauti yanayolimwa na wakulima kuanzia mboga mboga, nyanya, mahindi na mazao mengine, wakulima wanaweza kupata mbegu zinazokidhi mahitaji yao.

Amesema kampuni hiyo pia inapatikana na mbolea zenye viwango vya ubora kwa hatua mbalimbali za ukuaji wa mimea, ikiwemo mbolea za kuanzia, kuoteshea na kuzalisha, huku wakulima wakipata ushauri wa kitaalamu kuhusu aina ya mbolea inayofaa kulingana na zao na hatua ya ukuaji.

“Zao lolote linaloingia shambani, Asteria Agrovet tunalo,na kampuni yetu inalenga kuwa kituo cha suluhisho kwa mkulima anayehitaji pembejeo mbalimbali kwa ajili ya shughuli zake za kilimo.”amesema .

Ameongeza kuwa pamoja na mbegu na mbolea, Asteria Agrovet inauza pia viuatilifu vya kudhibiti wadudu pamoja na dawa za kuzuia na kutibu magonjwa ya fangasi, huku wataalamu wa kampuni hiyo wakiwa tayari kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya bidhaa hizo.

Zuhura amesema kupitia Maonesho ya Nanenane, wakulima wanapata fursa ya kufahamu bidhaa hizo kwa undani na kuona namna zinavyoweza kutumika shambani huku akiwataka wakulima wanaotembelea maonesho hayo kutumia fursa hiyo kupata elimu na ushauri kutoka kwa wataalamu wa kampuni hiyo.

Amesema Asteria Agrovet inapatikana Arusha, eneo la Stadium kabla ya makaburini, na inatoa huduma kwa jumla na rejareja kwa bei nafuu, huku ikiwakaribisha wakulima kutembelea duka lao na kupata bidhaa pamoja na ushauri wa kitaalamu.

Aidha, amesema kampuni hiyo inapatikana katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo TikTok, Facebook na Instagram kwa jina la Aseria Agrovet, huku wakulima wakialikwa kuwasiliana na kampuni hiyo kwa simu namba 0768 599 455, 0786 816901 na 0757 457229 kwa maelezo zaidi kuhusu bidhaa na huduma zinazopatikana.