Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Mkoa wa Temeke, Bw. Goodluck Assenga (kulia) akitoa ufafanuzi matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa Makamu Mwenyekiti wa Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu – Buza Bw. John Dede (kushoto) pamoja na waumini wa Parokia hiyo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya UWAKA 2026, yaliyofanyika leo Agosti 8, 2026 katika viwanja vya Parokia hiyo, Temeke, Dar es Salaam 

Mwenyekiti wa UWAKA Parokia ya Buza, Bw. Machowia Malisa (kulia) akipewa elimu ya matumizi ya luku na Afisa wa TANESCO Mkoa wa Temeke.

Wananchi wa Parokia ya Buza wakipewa elimu ya huduma mbalimbali za TANESCO

………..

Wananchi zaidi ya 150 wafurika Banda la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke na kupata elimu kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia, huku wananchi baadhi wakifanya manunuzi ya majiko hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya UWAKA 2026, Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu-Buza.

Maadhimisho hayo yaliyofanyika Agosti 8, 2026 katika viwanja vya Parokia hiyo, yamekuwa fursa kwa TANESCO Mkoa wa Temeke kutoa elimu kwa vitendo kuhusu matumizi salama ya umeme, nishati safi ya kupikia, matumizi ya mita za LUKU na huduma kwa wateja kupitia namba MCHONGO 180.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Mkoa wa Temeke, Bw. Goodluck Assenga, amesema lengo kuu lilikuwa kuhamasisha jamii kutumia nishati safi na rafiki kwa mazingira.

“Tumepika vyakula mbalimbali kwa kutumia majiko ya umeme ili wananchi wajionee jinsi ilivyo rahisi, salama na ya gharama nafuu. Tumefurahi kuona mwitikio mkubwa, watu wamekuja, wamejifunza na hata kununua,” amesema Bw. Assenga.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UWAKA Parokia ya Buza, Bw. Machowia Malisa, ametoa wito kwa familia zote kutumia nishati safi ya kupikia.

“Nishati safi ni rafiki kwa mazingira na inatusaidia kupunguza gharama za kupikia majumbani,” amesema.

Baadhi ya waumini wameshukuru TANESCO kwa elimu hiyo Bw. Greyson Komba amesema:

“Tumepata uelewa kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia, usalama wa umeme na matumizi ya LUKU majumbani.