Dodoma

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Alhaj Jabir Mussa Shekimweri, Agosti 06,2026 ametembelea banda la Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) katika Maonesho ya 88 ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Samuel Malecela, jijini Dodoma.

Akiwa katika banda hilo, Mhe. Shekimweri alipokea maelezo kutoka kwa viongozi na wataalamu wa VETA kuhusu mafunzo ya ufundi stadi, ubunifu wa teknolojia na huduma mbalimbali zinazotolewa na mamlaka hiyo kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira.

Pia alijionea bidhaa na kazi mbalimbali zilizobuniwa na wanafunzi wa VETA.