Na OWM-KAM – Dar es Salaam

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Zuhura Yunus, amewaaga rasmi vijana 531 wanaotarajiwa kwenda kufanya kazi katika nchi za Saudi Arabia, Qatar, Oman, Falme za Kiarabu (UAE), Ujerumani na Bosnia. Tarehe 30 Julai, 2026.

Akizungumza katika hafla hiyo, Zuhura amesema mafanikio hayo yametokana na juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kupanua masoko ya ajira. Amesema mafunzo ya uzoefu wa kazi (Internship) na uanagenzi yameendelea kuwa msingi muhimu wa kuwaandaa vijana wenye ujuzi, umahiri na ushindani unaohitajika katika soko la ajira la ndani na la kimataifa.

Aidha, ametoa wito kwa waajiri wa sekta ya umma na binafsi kuendelea kutoa nafasi za mafunzo kwa vijana ili kuongeza idadi ya Watanzania wenye ujuzi wa vitendo na kuwajengea uwezo wa kunufaika na fursa zinazojitokeza duniani.