Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameungana na Familia, Waumini, Viongozi na Wananchi mbalimbali katika Misa Takatifu ya kumbukumbu ya miaka sita tangu kufariki kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Benjamin William Mkapa, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Immaculate, UpangaDar es Salaam, leo tarehe 23 Julai 2026.