Na Mwandishi Maalum,Mbinga

TAASISI ya Kidoti Foundation chini ya Mkurugenzi wake Joketi Mwegelo kwa kushirikiana na Umoja Super Cup,imepanga kufanya ukarabati mkubwa wa uwanja wa mpira wa miguu wa Tazama uliopo kijiji cha Tanga Halmashauri ya Mji Mbinga.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kidoti Foundation Joketi Mwegelo Diwani wa kata ya Utiri Herswid Komba alisema,hatua hiyo itasaidia kuibua vipaji kwa vijana wa kijiji hicho na wilaya ya Mbinga kwa ujumla na itawezesha vijana kuonyesha vipaji vyao vilivyojificha na kupata nafasi ya kusajiliwa kwenye timu kubwa ikiwemo Simba na Yanga.