Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kigamboni, Bi. Tumaini Mahwaya (kulia) akitoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi  nishati safi ya kupikia leo  Julai 21, 2026  Soko la Ugindoni Mnadani, Kata ya Mji Mwema, Kigamboni, Dar es Salaam 

Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Wilaya ya Mikwambe, Godwin Marandu (katikati) akitoa elimu kwa wananchi kuhusu  umuhimu wa kutumia huduma za kidijitali za TANESCO, ikiwemo Luku Kijanja, MCHONGO 180 na NIKONEKT JISOTI, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na kuongeza ufanisi.

……….

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kigamboni limetoa elimu kwa wananchi wa Soko la Ugindoni Mnadani, Kata ya Mji Mwema, Kigamboni, Dar es Salaam kuhusu matumizi salama ya umeme, ul umuhimu wa kutumia nishati safi ya kupikia pamoja na  huduma za kidijitali za TANESCO, ikiwemo Luku Kijanja, MCHONGO 180 na NIKONEKT JISOTI, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na kuongeza ufanisi

Akizungumza leo Julai 21, 2026 wakati akitoa elimu hiyo, Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Kigamboni, Bi. Tumaini Mahwaya, amesema matumizi ya nishati safi ya kupikia ni muhimu si tu kwa afya za wananchi, bali pia kwa kulinda mazingira.

Bi. Muhwaya amesisitiza umuhimu wa kuzingatia usalama wa umeme majumbani na kutoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanaepuka matumizi hatarishi,

“Ni muhimu kutumia vifaa vya umeme kwa usahihi, ni hatari  kuunganisha umeme kiholela vinaweza kusababisha ajali kubwa,”

Aidha, ameeleza kuwa TANESCO itaendelea kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali ili kuwapatia elimu kuhusu huduma zake na kuhamasisha matumizi ya nishati safi, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuunga mkono ajenda ya taifa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Kwa upande wao Wananchi wameipongeza TANESCO Mkoa wa Kigamboni kwa  kutoa elimu hiyo muhimu. Wamesema elimu  hiyo imewaongezea uelewa kuhusu matumizi ya nishati ya umeme