Timu ya Taifa ya Hispania imefanikiwa kutwaa Kombe la Dunia 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Argentina katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa MetLife, New Jersey, Marekani.

Bao pekee la ushindi lilifungwa na mshambuliaji Ferran Torres katika dakika ya 116 ya mchezo.

Mchezo huo ulilazimika kuchezwa hadi dakika 120 baada ya dakika 90 za kawaida kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Argentina ilimaliza dakika 30 za nyongeza ikiwa pungufu uwanjani baada ya kiungo Enzo Fernández kuonyeshwa kadi nyekundu.