Mshiriki kutoka Uganda, Praise Wisdom, ametangazwa kuwa mshindi wa mashindano ya kusaka vipaji ya Bongo Star Search (BSS) msimu wa 16.
Kwa ushindi huo, Praise Wisdom amejinyakulia zawadi ya Shilingi milioni 50 pamoja na gari, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa uliomuwezesha kuibuka mshindi wa shindano hilo.
Ushindi wake umehitimisha msimu wa 16 wa Bongo Star Search, ambao uliwashirikisha washindani mbalimbali wenye vipaji vya uimbaji kutoka ndani na nje ya Tanzania.
