Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, ametembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Addis Ababa, Ethiopia, na kufanya mazungumzo na Mhe. Balozi. Innocent Shiyo.
Ziara hiyo imefanyika wakati Mhe. Salome akiwa nchini humo kushiriki Mkutano wa 22 wa Baraza la Mawaziri la Soko la Pamoja la Nishati Mashariki mwa Afrika (Eastern African Power Pool – EAPP), mkutano unaotarajiwa kuhitimishwa leo kwa kupitisha maamuzi muhimu kuhusu biashara ya pamoja ya umeme na uimarishaji wa gridi za taifa kati ya nchi wanachama.
Katika ziara hiyo, Mhe. Salome aliambatana na Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Mipango, Utafiti na Uwekezaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mha. HenryFried Byabato, aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Nishati.
