Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini DCEA, Aretas James Lyimo ametembelea banda la maonyesho la MSD, kwenye maonesho ya Biashara ya Kimatsifa Saba saba na kupata maelezo ya majukumu ya MSD ambapo alivutiwa na bidhaa za barakoa na mipira ya mikono zinazozalishwa na MSD.
Kamishna Lyimo amepongeza jitihada MSD kuanzisha kampuni Tanzu ya Medipharm, ambayo inasimamia viwanda vya MSD, kwani bidhaa muhimu zikipatikana nchini zinawarahisishia wadau na wateja wa MSD kupata kwa urahisi na bei nafuu.
“Hizi ni bidhaa ambazo wadau wengi hata kwetu tunazitumia, kuzalishwa nchini itarahisisha sana upatikanaji wake.” Alisema Kamishna Lyimo.

