KISIWANDUI, ZANZIBAR | 16 AGOSTI 2026
Katibu Mkuu CCM, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amempokea Katibu Mkuu SWAPO, kutoka Namibia, Ndugu Sophia Shaningwa, na kufanya naye mazungumzo katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Zanzibar.
Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha zaidi uhusiano wa kihistoria kati ya CCM na SWAPO, hususan kwa kuongeza ushirikiano na mafunzo ya uongozi kwa vijana, wanawake na taasisi za vyama.
Viongozi hao pia wamejadili umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kuendeleza mshikamano miongoni mwa vyama vya ukombozi vya Kusini mwa Afrika.

