Na Hellen Mtereko,Mwanza
Uwepo wa mazingira sahihi ya shule za kusomeshea watoto ni hitaji muhimu katika kufanikisha safari ya kimasomo kwa wanafunzi wanao hitimu darasa la saba kuweza kufanya vizuri.
Hayo yamebainishwa leo jijini Mwanza na wadau wa sekta ya elimu kwenye mahafali ya 10 ya darasa la saba katika shule ya Musabe Nursery and Primary Schools.
Akizungumza katika mahafali hayo Mdhibiti Ubora wa Elimu wilayani Nyamagana, Lucy Nyanda aliipongeza shule hiyo kwa kuwa na majengo yanayotosha kwa vyumba vya madarasa, maktaba na maabara kwa wanafunzi kuanza kutumia kwa elimu yao ya msingi.
Alisema shule kuwa na miundombinu ya kielimu ni nyenzo mhimu kuwezesha mzazi kufahamu ubora wa shule anayompeleka mwanaye.
Mkurugenzi wa Mwanza Uniform Felister Matoke wa Mkolani jijini hapa aliyekuwa ana mtoto anayehitimu Samir Mohamedi aliishukuru shule hiyo kwa kuweka mazingira mazuri ya kimasomo.
Alisema ataendelea kuhimiza watoto kuenenda katika tabia nzuri kama ambavyo wamekuwa wakifundishwa kwenye shule zao.
Mwalimu Gilbert Mahwaya wa shule hiyo mzazi wa Irene Mahwaya ambaye mwanaye alihitimimu alisema wanafunzi hao wanapaswa kujenga ukurasa mpya kimaisha.
Alisema wanafunzi wa kike ni kundi linalo hitaji kulindwa kwani wanaweza kutokufikia malengo yao maisha.
Christine Minja wa Nyashishi ambaye mwanaye Tiffany amehitimu aliipongeza shule hiyo kwa kuwaandaa wanafunzi waliohitimu darasa la saba kuanza elimu ya sekondari kwa kujiamini.
Naye Peter Mwanjoka wa Buhongwa mzazi wa Calister alisema katika kipindi ambacho wanafunzi watakuwa nyumbani kusubiria kuanza kidato cha kwanza watahakikisha wanaendeleza maadili mema waliyotoka nayo shuleni hapo.
Mama wa Nancy Peter, Dorca Salmon wa Nyegezi alishukuru malezi ya kitabia na kielimu ambayo mwanaye amepata hapo.

