Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Julai 7, 2026 amewasili kwenye Makao Makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris Nchini Ufaransa na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Profesa Khaled El-Enany, leo Julai 7, 2026.

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu yupo nchini Ufaransa kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Maadhimisho ya Tano ya Siku ya Kiswahili Duniani.