Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na ujumbe wa Kampuni ya Heidelberg Materials, ambao ni wazalishaji wa Saruji chapa ya Simba Cement na Twiga Cement, ulioongozwa na Mjumbe wa Bodi ya Uongozi na Mtendaji Mkuu wa Afrika, Mediterranean na Asia Magharibi, Bw. Hakan Gurdal, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Juni, 2026

Katika mazungumzo hayo, Kampuni hiyo imewasilisha mpango wa kupanua uwekezaji wake nchini, ukiwemo kuongeza uzalishaji wa Saruji, matumizi ya nishati safi na mradi wa usindikaji wa taka za majiji kwa ajili ya uzalishaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), aliyemaliza muda wake nchini Tanzania Mhe. Khalifa Abdulrahman Almarzouqi, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 26 Juni, 2026.