Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 30 imeamua kurudisha fadhila kwa jamii pamoja na walipa kodi kwa kufanya usafi katika stendi ya mabasi chalinze pamoja na kutoa vifaa mbali mbali vya usafi kwa wafanyabiashara pamoja na kutoa vyombo mbali mbali vya kupikia kwa wakinamama ambao ni mama lishe.
Katika msafara huo ambao uliongozwa na Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Zanzibar Salehe Haji Pandu amesema kwamba wameamua kwenda kuwatembelea wafanyabiashara wa chalinze kwa lengo la kuweza kuwasaidia ili waweze kuhakikisha wanapiga hatua katika kutimiza ndoto zao.
Aidha Naibu Kamisha huyo amebainisha kwamba Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kiasi kikubwa inawategemea Wafanyabiashara hivyo ni muhimu kuhakikisha wafanyabiashara wanakua huku nguvu kubwa wakielekeza kwa wafanyabiashara walio nje ya wigo Kodi ili kuongeza idadi ya Walipakodi wengine Wapya.
Kwa upande wake Meneja wa TRA Mkoa wa Pwani Peter Eliona amessema kwamba wataendelea kushirikiana bega kwa bega na na wafanyabiashara wote na kuwahimiza kuweka misingi ya kuweza kulipa kodi kwa wakati kwa lengo la kuiwezesha serikali kupata mapato yao.
Naye Meneja wa Stendi ya Chalinze Henry Mwalugenge akizungumnza kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Chalinze amewashukuru TRA Mkoa wa Pwani kwa kutoa elimu ya Mlipakodi katika eneo hilo pamoja Vifaa vya Usafi ikiwani mojawapo ya kutengeneza mahusiano mazuri na Walipakodi.
Akizungumnza kwa niaba ya Mama lishe Wa stendi ya mabasi chalinze,Mwenyekiti wa Mama lishe Bi.Zainabu Bakari amewashukuru TRA kwa kuwapa vifaa hivyo vitakavyo kwenda kuwarahisishia utendajikazi wao pamoja na kutengeneza mahusiano mazuri kwa walipa kodi.

