Timu ya watalaam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Juni 15, 2026 imeanza kutatua mgogoro wa malalamiko ya Kituo cha St. Charles Missionary Society, Tanzania wa kuzuiwa kuendeleza eneo lao Kiwanja Namba “794”, Kitalu “D” Mabibo katika Manispaa ya Ubungo jijini Dar es salaam.
Pichani, Mwenyekiti wa Wadhamini wa Kituo hicho, Sister Flossy Sequiere akiwa katika picha ya pomoja na Mwenyekiti wa Timu hiyo ambaye pia ni Msaidizi wa Waziri Mkuu Mahusiano, Asasi za Kiraia na Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Tryphone Mkolokoti (kulia) na Makamu Mwenyekiti ambaye pia ni Msaidizi wa Waziri Mkuu Masuala ya Ardhi, Senso Magessa baada ya mazungumzo ya awali ya kutatua mgogoro huo kwa maridhiano. yaliyofanyika kwenye nyumba ya Watawa hao, Bonyokwa jijini Dar es salaam.

