Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Pamba Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mabao ya Simba SC yalifungwa na Elie Mpanzu na Libasse Gueye, huku bao la Pamba Jiji likifungwa na Mathew Momanyi.

Simba imeendeleza ubabe wake kwa kuichapa Pamba Jiji na kuendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 61, nyuma ya vinara Young Africans S.C. (Yanga) wenye pointi 63.