Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi- (RUDN University) kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Profesa Oleg Yastrebov kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo Moscow nchini Urusi, tarehe 04 Juni, 2026. Rais Mhe. Dkt. Samia ametunukiwa Shahada hiyo ya Udaktari wa Heshima kutokana na mchango wake katika Mageuzi ya sekta ya Elimu, juhudi zake za kuimarisha Diplomasia ya Tanzania, pamoja na mchango wake katika kuimarisha hadhi ya Tanzania Kimataifa ikiwemo kupitia sekta ya Utalii,

Matukio mbalimbali wakati wa hafla ya kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa), kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi- (RUDN University), Moscow nchini Urusi, tarehe 04 Juni, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akicheza ngoma na Wanafunzi Watanzania wanaosoma katika Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi- (RUDN University), Moscow nchini Urusi, tarehe 04 Juni, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi wa Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi- (RUDN University), Wanafunzi wa Chuo hicho, wageni mbalimbali baada ya kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) kwenye hafla iliyofanyika chuoni hapo Moscow nchini Urusi, tarehe 04 Juni, 2026.