Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiteta jambo na Rais wa Benki ya Kiarabu ya Maendeleo Afrika-BADEA, Bw. Abdullah Kh Almusaibeeh, kando ya Mkutano Mkuu wa 61 wa mwaka 2026 wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Mkutano Mkuu wa 52 wa Mwaka wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki hiyo (ADF), unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kintélé, kilichoko nchini Congo Brazzaville.
BADEA ni miongoni mwa Taasisi za Fedha zenye mchango mkubwa wa maendeleo nchini Tanzania kupitia misaada na mikopo nafuu ikiwemo kuwa sehemu ya wadau waliochangia utekelezaji wa mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe , mkoani Kilimanjaro na Tanga, ulioghatimu shilingi bilioni 407.07, ambapo shilingi bilioni 244.10 zimetolewa na taasisi za fedha ikiwemo BADEA na kiasi cha shilingi bilioni 162 kilitolewa na Serikali ya Tanzania.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Congo Brazzaville)