…………

Shirika  la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kinondoni Kusini jijini Dar es Salaam limewakumbusha wateja wake hasa wateja wakubwa kuhakikisha wanalipa ankra za umeme (bill)kwa wakati.

Akizungumza katika kikao kati ya TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kusini na Wateja Wakubwa kilichokuwa na lengo la kujadiliana masuala mbalimbali Meneja wa TANESCO mkoa huo Adam Abdul ametumia bafasi hiyo kusisitiza ulipaji wa ankara za umeme kwa wakati ili kuwezesha shirika kuendelea kutoa huduma katika maeneo mengine.

“Tumekutana na Wateja Wakubwa katika mkoa wetu wa Kinondoni Kusini ,tumepokea changamoto zao na nyingi tumezifanyia kazi.Lakini nitumie nafasi hii kuwaambia wateja wetu wote walipe bill(Ankra)za umeme kwa wakati kwasababu zinapolipwa nasi zinatusaidia kufanya kazi na kuhakikisha upatikanaji wa umeme katika maeneo yote.”

“Kupitia kikao hiki wateja wetu wakubwa tumekubaliana wataendelea kulipa bill zao vizuri ,”amesema Abdull na kufafanua pia kwa sasa upatikani wa umeme umendelea kuimarika na hivyo kuondoa malalamiko kwa wateja wao.

Pia amesema kwa sasa TANESCO wanafanya kazi nzuri na malalamiko kwa wateja yamepungua na hata wateja wetu wakubwa katika kikao hawakuwa na malalamiko makubwa zaidi ya kuomba ankra kwa upande ziwahishwe ili nao walipe kwa wakati.

Kuhusu kikao cha TANESCO Kinondoni Kusini na Wateja Wakubwa,Abdull amesema kimekuwa na mafanikio makubwa na kwamba vikao vya namna hiyo ni endelevu kwani vinasaidia pande zote mbili kupata taarifa zenye lengo la kuboresha huduma.

Kwa upande wao baadhi ya wateja wakubwa waliohudhurika kikao hicho wametoa pongezi kwa TANESCO Mkoa wa Kinondoni Kusini kuandaa kikao ambacho kimewapa nafasi na kueleza yale ambayo wanaona yanakwenda kuboresha huduma za upatikanaji umeme.