Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, ameliomba Bunge kuidhinisha jumla ya Shilingi trilioni 4.286 kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

 

Dkt. Nyansaho amesema hayo leo Jumanne Mei 19, 2026 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

 

Amesema kati ya fedha hizo, Shilingi trilioni 3.859 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida huku Shilingi bilioni 426.53 zikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo.

 

Kwa mujibu wa Waziri huyo, bajeti hiyo inalenga kuimarisha sekta ya ulinzi kwa kuendelea kuboresha uwezo wa Jeshi kwa zana na vifaa vya kisasa, mafunzo, teknolojia pamoja na ustawi wa askari.