NAIBU Waziri ofisi ya Rais,menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora ,Regina Ndege Qwaray  akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan
………..
Na Happy Lazaro, Arusha
NAIBU Waziri ofisi ya Rais,menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora ,Regina Ndege Qwaray amesema kuwa wauguzi ni  watu wenye dhamana kubwa sana na wanategemewa  waendelee kuwa na kauli nzuri na nyuso zenye tabasamu na huruma kwa wagonjwa kwani hiyo ni tiba kwa wagonjwa.
Qwaray ambaye alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,Dokta Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo leo  wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani iliyofanyika katika ukumbi wa Aicc mkoani Arusha.
“Akitoka Mungu maisha ya mwanadamu yapo mikononi mwao na sisi  tukiumwa wa kutuhudumia ni nyie siwezi kujichoma sidhano mwenyewe .”amesema.
“Kuna baadhi ya mienendo ya wauguzi wanalalamikiwa na wananchi  kutokana na huduma wanazotoa tofauti na kiapo chao nawaomba sana  msiwe na nyuso za kikatili kwani  mkiwa hivyo mnawaongezea maumivu wagonjwa .”amesema
“Nawaomba sana msifanye wagonjwa wajutie kupata huduma kwenye vituo vya afya bali muwe na moyo wa ujasiri na upendo kwani mgonjwa anahitaji faraja kubwa sana kutoka kwenu tutoe huduma hii tukitegemea Mungu ametupa kibali hicho kupitia kwenu Taifa litakuwa limepona .”amesema.
“Kumekuwepo na malalamiko mengi sana kwenye wodi za wajawazito najua wauguzi mnapitia mengi ila nawaomba sana muwe na moyo wa ujasiri na upendo kwani mgonjwa anahitaji faraja kutoka kwenu.”amesema.
Qwaray  amewataka kuishi kwa mujibu wa viapo vyao ,kwani wao ndio wana hatma ya wagonjwa wao akitoka Mungu ni wao.
Aidha ameahidi kufanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolewa na wauguzi hao ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi unaotakiwa katika kutoa huduma inayostahili kwa wananchi.
Katibu mkuu wa TANNA Dokta Godfrey Chacha amesema kuwa ,kila  tarehe  12 Mei Dunia nzima huadhimisha siku ya Wauguzi; Tanzania kadhalika  hufanya maadhimisho haya ikiwa ni sehemu ya kutathmini huduma tunazozitoa, kukumbushana maadili ya taaluma yetu na kiapo cha Uuguzi katika kuwahudumia wagonjwa, kutoa elimu ya afya na kuhudumia wagonjwa/wateja na kuikumbusha  Serikali juu ya utekelezaji wa maazimio mbalimbali yaliyowasilishwa.
Amesema kuwa,Tunaona dhahiri juhudi za Serikali yetu ya Awamu ya sita chini ya uongozi makini  wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania na usimamizi wake thabiti katika kuboresha huduma za Afya Nchini.
“Miundombinu mbalimbali kujengwa,ajira kwa wauuguzi, bima ya afya kwa wote, Uboreshaji wa afya ya mama na mtoto nchiini na vifaa tiba katika hospitali  zetu ambayo ndiyo msingi wa huduma bora zitolewazo na Wauguzi, Kwa hili
Tunakushukuru sana kwa kuthamini afya za watanzania.”amesema dkt Chacha .
“Kutokana na umuhimu wa siku hii, sisi wauguzi nchini tumetoa huduma mbalimbali kwa wananchi katika.vituo vya afya na hospitali ndani ya mkoa wa Arusha na  kufanya jumla ya wananchi
waliopata huduma kuwa 84,149.zoezi hili limetusaidia kubaini wateja ambao
wapo kwenye visababishi hatarishi na kuwapa ushauri wa kitaalamu.
Amefafanua kuwa,kupitia  Kongamano la Kimataifa la kisayansi ambalo wauguzi walipata  fursa ya kujadili tafiti mbalimbali zilizofanywa na wauguzi pamoja na wadau wengine wa afya juu ya utoaji wa huduma bora za afya ili kuboresha huduma za afya nchini.
“Tulifanya pia Mkutano Mkuu wa Chama ambapo tulipata fursa ya kujadili
mambo mbalimbali yanayohusu taaluma yetu na kufanya tathmini ya
tulikotoka, tulipo na tunakotaka kufika na kukubaliana maazimio ya utoaji wa
huduma kwa weledi na kuboresha huduma za Uuguzi nchini na kutuweka
wauguzi pamoja kifikra na kimtazamo kwa mustakabali wa taaluma kwa faida
ya wananchi wa Tanzania.”amesema dokta Chacha.
“Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Muasisi wa Uuguzi Duniani kila mwaka huwa na Kauli mbiu ambayo hubeba ujumbe maalum, kwa Mwaka huu 2026 kauli mbiu  hiyo inasema: “WAUGUZI WETU, MUSTAKABALI WETU, WAUGUZI
WALIOWEZESHWA HUOKOA MAISHA” ambapo kauli mbiu hii inataka jamii na viongozi kuwaheshimu wauguzi kama viongozi,  waelimishaji, na watetezi wa afya ya jamii.
Inaonyesha Uuguzi ni taaluma muhimu  ya kimataifa inayolenga kutambua, kuthamini, na kuwekeza katika kada ya uuguzi  ili kuboresha afya za jamii na uchumi kwa ujumla.”amesema
“Wauguzi ni uti wa mgongo wa mfumo wa afya. Wao ndio wahudumu wa kwanza na wa muda mrefu zaidi kwa mgonjwa, kuanzia hatua za mwanadamu hadi mwisho  wake.”amesema Dokta Chacha.
Ameongeza  kuwa,TANNA imefanikiwa kuimarisha utawala bora kwa kupata
uongozi mpya utakaokaa madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu yaani
2025-2028 unaolenga kutetea maslahi ya wauguzi na kuboresha utendaji.
Naibu Waziri anaeshughulikia masuala ya afya TAMISEMI Dokta Jaffar Rajabu amesema Serikali imeendelea kufanya maboresho makubwa katika sekta ya afya ikiwemo kuongeza nguvu katika huduma za uuguzi na ukunga ili kuboresha huduma kwa wananchi.
Maadhimisho hayo yamewakutanisha viongozi wa Serikali, wataalamu wa afya pamoja na wauguzi na wakunga kutoka maeneo mbalimbali nchini kujadili maendeleo na changamoto za taaluma hiyo.