Klabu ya Espérance Sportive de Tunis imetangaza kuachana na kocha Patrice Beaumelle, kwa uamuzi uliotekelezwa mara moja. Hatua hii imekuja baada ya mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha yaliyoiacha klabu hiyo bila taji msimu huu.
Sababu zilziopelekea kuondoka kwa kocha huyo raia wa Ufaransa:
Espérance iliondolewa katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Mamelodi Sundowns kwa jumla ya mabao 2-0.
Kipigo cha 1-0 dhidi ya wapinzani wao wakubwa, Club Africain, juzi Jumapili, Mei 10 kiliwafanya mahasimu wao hao kutwaa ubingwa wa Tunisia msimu wa 2025/26.
Beaumelle, aliyekuwa klabuni hapo tangu Februari, ameshuhudia timu ikipoteza kasi muhimu katika kipindi cha lala salama cha msimu.
Klabu hiyo imemtangaza Christian Bracconi kuwa kocha wa muda atakayekiongoza kikosi hicho hadi mwisho wa msimu huu.
