TRA United imepata sare ya bao 1-1 kwenye uwanja wake wa nyumbani dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa ligi uliochezwa leo.
TRA United ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Joseph Akandwanaho dakika ya 20 ya mchezo.
Hata hivyo, JKT Tanzania ilisawazisha dakika ya 30 kupitia kwa Salum Hamis.
Matokeo hayo yanaifanya TRA United kubaki nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 34, huku JKT Tanzania ikishika nafasi ya tano kwa pointi 36.
