*Akutana na Wanamichezo wa Timu ya maliasili wanaoshiriki Mei Mosi Njombe
*Awaasa wanamichezo wa Timu ya Maliasili kuhakikisha wanadumisha michezo mahali pa kazi
*Azipongeza timu za Kamba wanaume kwa kutinga nusu fainali, na medali saba kwenye michezo mbalimbali
Na Neema Thomas Chalila, Njombe
Mkurugenzi msaidizi wa Utawala (ADA) kutoka Wizara ya Maliasili na utalii Bi. Vailet Mlinga ameitaka Timu ya Maliasili na Utalii inayoshiriki Mei Mosi kuhakikisha inadumisha Nidhamu na Maadili na uwajibikaji kwani ndio msingi wa ushindi michezoni.
Bi Mlinga ameyasema hayo kwenye kikao na wanamichezo wa Wizara ya Maliasili na Utalii wanaoshiriki michezo ya Mei Mosi Mkoani Njombe, kwa lengo la kujionea namna Wizara inavyoshiriki michezi ya Mei Mosi 2026.
Aidha amewapongeza wanamichezo wote kwa kuweka nguvu moja na kuweka bidii kwenye michezo na kuhakikisha wamefika robi fainali, nusu fainali kwenye michezo mbalimbali na kuipongeza timu ya kamba kwa upande wa wanaume kwa kufika nusu fainali.
Wizara ya Maliasili na Utalii kwa upande wa michezo ya meimosi iliwakilishwa na michezo ya Mpira wa pete, miguu, kamba kwa wanawake na wanaume, Darts,riadha,Bao,na michezo mingine ya jadi.
Ameahidi kuzifanyia kazi changamoto zote zilizojitokeza wakati wote wa mashindano ya mei mosi na kuzipatia ufumbuzi.





