Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Muungano baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mlandege FC katika mchezo uliopigwa leo, Aprili 26, 2026, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Simba SC walifanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya 63 kupitia kwa mshambuliaji wao, Selemani Mwalimu, baada ya kupokea pasi kutoka kwa Clatous Chama.
Dakika ya 76, Simba SC walipata bao la pili kupitia kwa Anicet Oura na kuzima matumaini ya Mlandege FC kutinga hatua ya fainali. Bao la tatu lilifungwa na Neo Maema.
Kufuatia matokeo hayo, Simba SC itacheza na Yanga SC katika mchezo wa fainali ya kombe hilo utakaopigwa Aprili 29, 2026, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Mara ya mwisho Simba SC ilikutana na Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo walitoka sare tasa ya bila kufungana.




