Baadhi ya walimu wanawake ambao ni wanachama wa Chama cha walimu(CWT)walioshiriki bonanza la michezo wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Ruvuma Kalimeje Sandali(hayupo pichani)kwenye uwanja wa michezo wa ccm Tunduru mjini
Na Mwandishi Maalum,Tunduru
WALIMU wanawake wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT)wilayani Tunduru,wamefanya bonanza la michezo mbalimbali lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Chama cha Mapinduzi Tunduru mjini.
Mratibu wa bonanza hilo Evodia Makota alisema,lengo ni kufanya bonanza hilo kuwakutanisha walimu wanawake wanawake ili watambuane,kupata burudani sambamba na kutoa elimu ya chama,ujasiriamali na waweze kujitambua kwenye chama cha walimu na sekta nzima ya walimu.
Alitaja michezo iliyofanyika katika bonanza hilo ni kufukuza kuku,mpira wa pete,kukimbia kwenye magunia,kuvuta kamba,kujaza maji kwenye chupa kwa kutumia mdomo.
Baadhi ya walimu,wamekipongeza Chama cha walimu(CWT) wilaya ya Tunduru kwa kuandaa bonanza hilo ambalo limewezesha kuwakutanisha pamoja walimu wanawake na viongozi wa chama chao.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Makaukau alisema,wamefurahi kukutana na walimu wenzao wanawake na kushiriki michezo mbalimbali kwani kutokana na majukumu yao wanakosa nafasi ya kushiriki michezo au kukutana na walimu na kufahamiana na kushirikiana katika mambo mbalimbali.
“bonanza hili la leo limetufanya kuwa majasiri na tunaamini kama walimu wanawake tunaweza,kwa sababu jamii yetu inatuangalia sisi kama walimu kulea kwa kzazi kinachokuja”alisema
Aidha alisema,wanajivunia kuwa wanachama wa Chama cha walimu Tanzania(CWT)ikiwemo kushiriki michezo mbalimbali,kusaidiana pale mmoja anapokuwa na shida na kupata fursa ya kujifunza.
Naye mratibu elimu kata ya Mlingoti Shida Nyenje alisema,wamefurahi kushiriki bonanza hilo kwani limesaidia sana kuwakutanisha walimu wanawake wa wilaya ya Tunduru.
Nyenje alisema,Chama cha walimu(CWT)ni chama kikongwe na walimu wanajivunia kuwa wanachama ambapo amewaomba walimu ambao sio wanachama kuhakikisha wanajiunga.
Katibu wa Chama cha walimu Tanzania(CWT)Mkoa wa Ruvuma Rashid Mchekenje,akizungumza na walimu wanawake wa wilaya ya Tunduru kwenye bonanza maalum la michezo lililofanyika katika uwanja wa CCM Tunduru mjini.
Baadhi ya walimu wanawake ambao ni wanachama wa chama cha walimu Tanzania(CWT)wakishiriki mazoezi ya viungo kwenye bonanza lililofanyika katika uwanja wa michezo wa CCM Tunduru mjini.
Walimu wakishiriki mchezo wa kuvuata kamba.
PWalimu wakikimbia kwenye magunia wakati wa bonanza maalum la walimu wanawake katika uwanja wa michezo wa CCM Tunduru mjini.




