Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Constantine Sima, ambaye ndiye Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa nchini (ALAT) akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha
………
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Katika kuhakikisha wanawake wanaondokana na changamoto ya mitaji Kafiti Foundation iliyopo Ilemela Jijini Mwanza imekuja na mpango wa Kafiti na mwanake kwaajili ya kutatua changamoto hiyo.
Hayo yamebainishwa leo Ijumaa Aprili 24, 2026 na Mkurugenzi wa Kafiti Foundation, Mhandisi Mapuli Kafiti wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea kwenye Kongamano la Kafiti na mwanamke litakalofanyika kesho Aprili 25, 2026 katika Hoteli ya Malaika Jijini Mwanza.
Amesema wanawake wengi nchini wanafanya kazi kubwa lakini wanakutana na changamoto kuu tatu.
“Upatikanaji mdogo wa mitaji,ukosefu wa mifumo rasmi ya kukuza biashara pamoja na ukosefu wa ulinzi wa kifedha wa muda mrefu, hivyo kafiti Foundation imeamua kuingia si kama mshiriki bali kama mtekekezaji wa suluhisho”,
Amesema kupitia mpango huo wa Kafiti na Mwanamke, zaidi ya wanawake 3,000 watanufaika moja kwa moja kupitia uwezeshaji wa mitaji kwaajili ya biashara ndogo na za kati,upatikanaji wa vifaa vya uzalishaji kama gesi kwa mama lishe na bajaji kwa wanawake na vijana.
“Mafunzo ya ujasiriamali na elimu ya fedha,fursa za masoko na mitandao ya kibiashara,huduma za afya na uchunguzi wa awali elimu ya bima na hifadhi ya jamii huu ni mfumo unaolenga matokeo siyo nadharia”, Amesema Kafiti.
Aidha, amesema kuwa CRDB Bank Foundation wanakuja na nguvu ya kifedha kuhakikisha wanawake wanapata mitaji na maarifa ya kusimamia fedha zao huku NSSF wakihakikisha uwezeshaji huo hauishii kwenye kipato cha leo bali unaweka msingi wa usalama wa kesho kupitia hifadhi ya jamii.
Kwaupande wake Meneja wa Kanda Benki ya CRDB, Denis Mwoleka amesema watashirikiana na Kafiti Foundation kuhakikisha wanawawezesha wakinamama mitaji itakayosaidia kuinua vipato vyao.
Naye Meneja wa NSSF Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Kahensa amesema watashiriki kikamilifu kwenye kongamano hilo kwaajili ya kutoa elimu na wale wenye sifa wapata fursa ya kujiunga na mfuko huo.




