Na. Gladys Lukindo- BMH
MANYARA – APRILI 23, 2026
Daktari Bingwa wa Upasuaji, Sandra Sillas aliye mfanyia upasuaji amesema binti huyo amekuwa akipata maumivu makali yanayo kuja na kupotea.
“Uvimbe huu tuliotoa ulikuwa mgongoni (huge back tumour) ambao una kilo mbili,” alisema Dkt. Sandra.
Ameongeza kuwa kama uvimbe huu usingetolewa ungemletea madhara na ungepelekea saratani.
“Kama uvimbe huu usinge tolewa ungeendelea kukuwa na matokeo yake ungepelekea kuwa saratani, uvumbe huu tulioutoa amekaa nao kwa zaidi ya miaka kumi “ amesema Dkt. Sandra.
Kwa upande wake , mgonjwa huyo aliyefanyiwa upasuaji ameishukuru Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa huduma hiyo ya matibabu.
“Nawashukuru madaktari wa Benjamin Mkapa kwa huduma nzuri kabla ya operation nilikuwa siwezi kulala vizuri na hata siwezi kuegemea vizuri lakini sasahvi naendelea vizuri,” ameongeza.
Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa wameweka kambi katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Manyara ikiwa ni sehemu ya kusogeza na kuhudumia wananchi wenye uhitaji.




