Na HENRI SHAABAN, DAR ES SALAAM
Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Mwalimu Dkt.Mussa Ally, amepewa tuzo na shule ya Sekondari Mvuti iliyopo wilayani Ilala kwa usimiaji mzuri sekta ya Elimu Idara ya Elimu Sekondari kupelekea shule za Sekondari Ilala kufanya vizuri katika matokeo yake kila mwaka.
Tuzo hiyo Mwalimu Dkt.Mussa Ally , alipewa katika mahafali ya kwanza ya kidato cha sita shule ya Mvuti Sekondari Wilayani Ilala ambapo jumla ya Wanafunzi 48 walipewa vyeti vya kuhitimu kidato cha sita.
Akizungumza katika mahafali ya kwanza ya kidato cha sita Mkuu wa shule ya Mvuti Sekondari Mwalimu Gasper Mwaipopo alisema wamemkabidhi tuzo Dkt.Mussa Ally kutokana na mchango wake mkubwa kumsaidia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Sekta ya elimu Idara ya Elimu Sekondari ameweza kufanya mambo makubwa ya ufaulu na kukuza Taaluma Ilala.
Mwaipopo alisema katika shule za Wilaya ya Ilala kiwango cha taaluma kimeongezeka na sasa kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Elihuruma Maberya idara ya Sekondari imeweza kujenga shule za Sekondari za kisasa zimekamilika na zingine zinajengwa kiwango cha magorofa.
“Tuzo hii tumemzawadia Mkuu wetu wa Idara ya Sekondari ni alama tosha mchango mkubwa anaofanya Wilayani Ilala katika idara ya Sekondari kwa kushirikiana na Serikali “alisema Mwaipopo.
Mwalimu Mwaipopo akizungumzia mahafali ya kwanza ya Sekondari ya shule ya Mvuti alisema jumla ya wanafunzi 48 wanatarajia kufanya mitihani yao ya Taifa hivi karibuni ambapo wanafunzi hao wamefanya vizuri katika mitihani yao ya moco na mitihani ya kujipima.
Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Dkt. Mussa Ally alitumia fursa hiyo kuwapongeza shule ya sekondari Mvuti kwa kufanya vizuri katika mitihani yao ya kujima Moco hivi karibuni ambapo alisema wanafunzi hao wote waongeze bidii watapata Division one .
Dkt Mussa Ally aliwataka Wanafunzi hao wakajiandae vizuri n mitihani yao na kuchangamkia fursa za masomo mbalimbali.
Aidha aliwataka huo wanapoenda wakawe mabalozi wazuri katika kwenda kuitangaza shule hiyo ya Sekondari Mvuti ambayo hivi karibuni itakuwa ya vipaji maalum na Bweni kwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa sana kuwekeza katika shule mvuti.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Msongola Magdalena Thomas aliwataka Wazazi wa na Walimu wa shule ya sekondari Mvuti kushirikiana pamoja na wanafunzi wa shule hiyo kwa ajili ya kuongeza ufaulu.
Diwani Magdalena Thomas alisema katika ya Msongola anajivunia kupata shule hiyo ambayo ina wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka kidato cha sita na hivi karibuni inakuwa ya vipaji maalum pamoja na bweni .
Aliwataka Wazazi katika jimbo la Kivule kujivunia shule hiyo kazi iliyofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa Ilani katika sekta ya Elimu.





