‎Marehemu William Vangimembe Lukuvi alizaliwa Agosti 15, 1955 katika kijiji cha Mapogoro, mkoani Iringa.

‎Alisoma elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Kitanewa kuanzia mwaka 1962 hadi 1970, kisha kujiunga na Chuo cha Ualimu Tabora (Tabora TTC) kati ya mwaka 1974 hadi 1975 ambapo alihitimu na kuwa mwalimu. Baada ya hapo alifanya kazi ya ualimu kabla ya kuingia kwenye siasa.

‎Aliingia rasmi katika siasa mwaka 1995 alipochaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Ismani, nafasi aliyodumu nayo kwa zaidi ya miaka 30 mfululizo hadi kifo chake.

‎Katika utumishi wake serikalini, alihudumu katika nyadhifa mbalimbali. 

Kuanzia mwaka 2010 hadi 2015, alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge). Baadaye, kuanzia mwaka 2015 hadi 2022, aliteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambapo alisimamia kwa ukaribu masuala ya ardhi nchini.

Mwaka 2023, aliteuliwa kuwa mshauri wa Rais katika masuala ya kisiasa na kijamii, kabla ya kurejea tena serikalini na kushika nafasi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), nafasi aliyokuwa akiitumikia hadi mwisho wa maisha yake.

Mnamo Machi 25, 2026, taarifa za kifo chake zilitangazwa rasmi na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, zikieleza kuwa Hayati Lukuvi amefariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma, kutokana na matatizo ya moyo.

Kifo chake kimehitimisha safari ya kiongozi aliyepitia ngazi mbalimbali za uongozi, kuanzia mwalimu, mbunge hadi kuwa mmoja wa mawaziri waliodumu kwa muda mrefu serikalini.

‎( Hii ni Fullshangwe Blog, Update Kitaifa) 

‎imeandikwa na kuandaliwa na Meleka Kulwa- Dodoma 

‎Chanzo: Parliament of Tanzania – CV ya Mbunge)